SANCHI hana kovu la kiwembe

KWELI? Mrembo ambaye jina lake limesimama kutokana na umbo lake matata, Jane Rimoy ‘Sanchi’ hivi karibuni alionekana akijiachia huku akiwa amevaa nguo za kuogelea huko visiwani Zanzibar na kufuta ule uvumi kwamba alichanwa viwembe.

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Sanchi alisema tangu azushiwe kuwa alichanwa na viwembe baada ya kufumaniwa na mume wa mtu hivi karibuni, hajawahi kuwadhihirishia watu kuwa hana kovu hata moja kwenye mwili wake bali watu walikuwa wakijifurahisha kuongea.

“Wale wote waliokuwa wakidai nimechanwa mwili, sitamaniki, basi waangalie halafu wakiona kama nina kovu lolote, waniambie maana watu wanaweza kukuzushia kitu bila sababu,” alisema Sanchi.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Toa comment