Sanchi: Picha za Utupu Ziliniumiza Sana

HIVI karibuni wimbi la picha za utupu za warembo mbalimbali kusambazwa mitandaoni limezidi ambapo zinawaletea athari kubwa katika maisha yao ya kila siku. Picha hizi zimekuwa zikivujishwa aidha na wao wenyewe au wanaume wanaojihusisha nao kimapenzi.
Mrembo Jane Rimoy “Sanchi” ni mmoja wa mrembo ambaye amekumbana na fedhea hiyo ambapo kila mmoja anaamini kuna mchezo mchafu alichezewa na mtu wake wa karibu au hata adui ili tu kuivua heshima yake kwenye jamii.
Gazeti la Amani lilimtafuta na kufanya naye mahojiano maalum kuhusiana na skendo hiyo ya picha za utupu zilizovuja mwishoni mwa mwaka jana na kufunguka kama ifuatavyo;
Amani: Habari Sanchi, pole na misukosuko.
Sanchi: Nimeshapoa, unajua katika maisha lazima ukutane na changamoto kama hiyo ili upate cha kujifunza na kuadithia.
Amani: Ilikuwaje mpaka kupiga picha za namna ile?
Sanchi: Kwa kweli ni stori ndefu kwa sababu hata picha zenyewe ni za muda mrefu lakini kuna nyingine ambazo siyo zangu pale.
Amani: Kwa hiyo una maanisha aliyefanya hivyo ni mtu wako ambaye ulikuwa naye?
Sanchi: Hapana kabisa, kwa sababu mtu wangu hawezi kufanya hivyo na kwa nini afanye hivyo, najua ilikuwaje lakini siwezi kuanika hapa.

Amani: Vipi ulijisikiaje sasa baada ya kuona zinazidi kusambaa mitandaoni? Sanchi: Kwa kweli kama binadamu lazima niumie sanasana lakini sikuwa na jinsi kwa sababu mitandao inasambaa kwa haraka sana, niliamua kukaa tu kimya.
Amani: Vipi kuhusu familia hasa mama mzazi? Sanchi: Familia yangu haikuwa na shida kwa sababu wanajua ni vitu vya zamani sana.
Amani: Ushachukua hatua yoyote kwa sasa? Sanchi: Ndiyo ila ni siri yangu.
Amani: Kutokana na picha hizo na video kusambaa, hazikufanya ushindwe kwenda mahali au kutoka nje?
Sanchi: Hapana, nilikuwa nafanya vitu vyangu kama kawaida kwa sababu mwisho wa siku lazima maisha yaendelee.
Amani: Kuna picha ambazo ulizikana kwamba siyo wewe, hiyo ikoje ? Sanchi: Yaani kwa watu wanaonifahamu kiundani, watajua tu si mimi niliyekuwa naonekana kwenye baadhi ya picha.

Amani: Nini umejifunza katika hili? Sanchi: Kutomuamini kila mtu hata kama ndugu yako. Amani: Najua una mpenzi, na yeye ana ndugu zake walilichukuliaje hilo?
Sanchi: Ni waelewa sana na wala hawafuatilii vitu kama hivyo. Amani: Nini unachotaka kuwaambia baadhi ya wanawake au mastaa wenzako wa kike?
Sanchi: Kuwa makini na kila kitu siyo kila mtu anawapenda. Amani: Vipi kuhusu duka lako la Seductive unatarajia lini kulifungua.
Sanchi: Hivi karibuni, watu wakae tu tayari. Amani: Kwa mwaka huu mpya nini malengo yako? Sanchi: Malengo yangu ni kuwa mwanamitindo wa kimataifa.
Amani: Shukurani kwa muda wako. Sanchi: Asante sana, karibu.
Makala: IMELDA MTEMA

