SANCHI: SIJAONA MWANAUME BONGO

Jane Rimoy ‘Sanchi’

MWANAMITINDO Jane Rimoy ‘Sanchi’ ameibuka na kusema kuwa, hajaona mwanaume wa kuwa naye kimapenzi Bongo japo karibia mastaa wote wenye majina makubwa wamemtongoza.  

 

Akipiga stori na Amani, Sanchi alisema kuwa kama angetaka kuwa na uhusiano na mwanaume wa Kibongo angefanya hivyo lakini hajaona mwanaume wa kuwa naye na wala hawashobokei kwani kama ni wanaume wamejaa kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao humfuata kwa njia ya meseji za moja kwa moja.

 

“Unajua mimi siwezi kuwashobokea kabisa wanaume wa Kibongo kama kunitongoza wamenitongoza sana, si hao tu hata wanaume wa nje tena mastaa Marekani, wanamuziki na wanamichezo wamekuwa wakinisumbua sana na sijawa na uhusiano nao sembuse hao wa Kibongo siwataki,” alisema Sanchi.

Aidha, mrembo huyo mwenye figa matata alidai kuwa watu wamekuwa wakimsumbua na kumuuliza kama hajatongozwa na msanii mkubwa anayeongoza kwa sasa Bongo (jina kapuni) na kuwataka watambue kwamba msanii huyo aliwahi kumtongoza lakini hakumkubalia.

 

“Huyo msanii wao alishanitongoza na nikamkataa, si huyo tu wasanii karibu wote wakubwa Bongo wameshanitaka nikawakatalia, siwataki. Wenye hamu ya kumjua mtu wangu ipo siku nitamuanika,” alisema Sanchi ambaye hivi karibuni alipata dili la kutangaza mbwa wa majumbani ambapo amekuwa akitupia picha mbalimbali zinazoonesha akiwa na mbwa hao katika mtandao wa Instagram.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Loading...

Toa comment