The House of Favourite Newspapers

Sancho Azuiwa Kufanya Mazoezi Na Kikosi Cha Kwanza Cha Man United

0

Klabu ya Manchester United imetangaza kuwa winga Jadon Sancho ameondolewa kwenye kikosi cha kwanza maana yake atafanya mazoezi binafsi nje ya kikosi cha Mashetani hao Wekundu.

“Sancho atasalia kwenye programu ya mazoezi ya kibinafsi mbali na kikosi cha kwanza huku akisubiri suluhu juu ya suala lake la kinidhamu” imesema taarifa ya United.

Itakumbukwa nyota huyo raia wa England alimjibu wazi wazi kocha Eric Ten Hag baada ya meneja huyo kudai hajafanya vya kutosha mazoezini ndio maana hakumchagua katika kikosi kilichopokea kichapo cha 3-1 dhidi ya Arsenal.

Mtwara: RAIS SAMIA ATINGA AIRPORT ya MTWARA KUSHUHUDIA KAZI KUBWA ILIYOFANYIKA…

Leave A Reply