The House of Favourite Newspapers

Sangoma wa Hamisa ni Kiboko

0

SANGOMA wa Hamisa ni kiboko! Hizo ndizo kauli zinazotolewa na baadhi ya mashabiki wa mwanamitindo Hamisa Mobeto wakimaanisha kwamba huwenda kuna mganga (sangoma) anayemfanya nyota yake ing’ae na mambo yake kumuendea swadakta.

 

“Jamani siku hizi Hamisa (Mobeto) hakamatiki, madili kama yote, hao wanaume sasa wanavyompapatikia ndiyo usiseme, huyu lazima ameenda kwa mganga, ninyi wenyewe mashahidi, angalieni alivyokuwa mwanzo na sasa; yaani vitu viwili tofauti,’’ anasema mmoja wa Team Hamisa kwa sharti la kutotajwa gazetini.

 

IJUMAA KAZINI

 

Baada ya mambo kuzidi kuwa mengi, huku kila mmoja akizungumza lake, Gazeti la IJUMAA liliingia kazini na kufanya uchunguzi ambapo lilibaini anayemng’arisha Mobeto si mwingine bali ni nyota yake kali aliyonayo na wala si vinginevyo.

 

Mobeto amezaliwa Disemba 10, 1994 na aina ya nyota yake ni Mshale ambapo kwa mujibu wa mtaalam wa nyota, watu wenye nyota hii ni waaminifu na wanaopenda mno mafanikio hivyo hujituma zaidi kwenye kazi na kutimiza malengo yao kirahisi.

 

TUIJUE NYOTA YA MOBETO

 

Nyota hiyo ya Mshale ambayo ni ya Mobeto, ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12.

 

Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 23, Novemba na 20, Disemba au wenye majina yanaoanza na herufi I na U.

 

Asili yao ni Moto na siku yao ya bahati ni Alhamisi, namba yao ya bahati ni 3 na Sayari yao ni Jupiter (Mushtara).

 

Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeell na Jini anayetawala Alhamisi anaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor.

 

Herufi ya Alhamisi ni DH, inayoelezwa pia kuwa rangi inayowapa uwezo wa kipato ni nyeusi na bluu iliyoiva.

 

Matakwa yao ni kupanuka kimawazo; inasemekana pia katika kazi na biashara watu wenye nyota ya Mshale ni waaminifu na wanaopenda mafanikio ambao wako tayari wakati wowote katika kazi.

 

Kutokana na kupenda kufanya kazi kwa bidii, wana bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.

 

Wenye nyoya ya Mobeto ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi, wao wanaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.

 

Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria; uandishi, ualimu, dini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.

 

TABIA ZAO KIMAPENZI

 

Katika mapenzi ni wachangamfu na wenye kupenda, lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.

 

Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu; mwanzoni wanakuwa wagumu kujihusisha na mambo hayo, lakini wanapenda wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.

 

Wapenzi wao wanapoonesha dalili ya kuwapenda, basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.

 

MAFANIKIO YA MOBETO

 

Kwa kipindi cha muda mfupi, mwanamama Mobeto ameweza kujizolea madili mengi na kujinyakulia mkwanja mrefu ambapo anasema kuwa, siri kubwa ya kufuatwa na kampuni tofauti ni kuwa mwaminifu katika kazi anayopewa.

 

Miongoni mwa madili aliyonayo ni pamoja na dili la sabuni, nywele, jezi, pikipiki, taulo za kike, kodi na mengine kibao.

 

MOBETO NA NYOYA YA MASTAA WA KIUME

 

Mbali na madili, Mobeto siku hizi ameingia kwenye skendo ya kufuatwafuatwa na mastaa wakubwa ndani na nje ya nchi kama rapa mkali wa Marekani, William leonard Robets ‘Rick Ross’, Davido Adedeji Adeleke ‘Davido’ wa Nigeria na wengineo, kiasi kwamba hadi wanawake wenzake wanamuonea donge bila kujua yote hayo yanatokana na nyota aliyonayo.

 

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply