The House of Favourite Newspapers

Sarah Mvungi: Nina gundu na wanaume

0

MAHARIYAFLORAMVUNGI1.jpgBRIGHTON MASALU

MSANII wa muziki wa Injili, Sarah Mvungi amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa ana gundu na wanaume na kwamba wengi humkimbia kutokana na sharti analowapa.

Akizungumza na Amani, Sarah alisema katika maisha yake hajawahi kufurahia mapenzi, aliwahi kuishi kwenye ndoa kwa miaka 12 lakini hakuwahi kufurahia maisha ya kuolewa.

“Si kwamba sitongozwi, la hasha, natongozwa tena wengi wanakuja kwa gia ya kutaka kunioa lakini kila mwanaume anataka kushiriki tendo la ndoa kwanza kabla ya ndoa, jambo ambalo sipo tayari kuliruhusu kwa kuwa mimi ni mtumishi wa Mungu mwenye hofu ya dhambi.

“Mwanaume nikimpa sharti hilo, anakimbia na harudi tena, yaani ni kama nina  gundu lakini naamini Mungu atanipa mwanaume wa kuendana na mimi,” alisema Sarah.

Leave A Reply