The House of Favourite Newspapers

Sarah wa Harmo Awachefua Warembo Uganda

0

KWA matarajio yao, baadhi ya warembo wa Kiganda walifikiri staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ atazuru nchi hiyo akiwa peke yake, badala yake akatimba na mkewe, Sarah Michelotti, unaambiwa walichefukwaje?

 

Iko hivi; mwishoni mwa wiki iliyopita, Harmonize au Harmo alikwea pipa la Uganda Airline aina ya Bombardier CRJ900 na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe International Airport, Kampala kwa ajili ya kuhudhuria shoo ya miaka 10 ya mchekeshaji maarufu nchini humo aitwaye Patrick Salvador Idringi.

 

Taarifa kutoka Uganda zinaeleza kuwa, watoto wazuri wa Kiganda waliposikia Harmo anatimba, walitaka kuitumia chansi hiyo kama fursa ya kujilengesha kwake kimapenzi maana walishajua siku hizi hatembei na mkewe.

 

“Walikuwa wanamfuatilia kwa umakini mno kwenye Insta (Instagram) wakaona Harmo siku hizi anatembea peke yake bila Sarah, sasa waliposikia anakuja Uganda, wakawa wanamlia mingo kwenye hoteli aliyofikia,” kilimwaga ubuyu chanzo makini kutoka nchini Uganda.

Lakini Harmo aliwasapraizi warembo hao baada ya kushuka kwenye ndege akiwa na mkewe pamoja na mabaunsa.

Bahati mbaya ni kama alijua, Sarah alijibebisha kwelikweli kwa kumshika mkono Harmo kila walipokuwa, kuanzia uwanja wa ndege hadi kwenye hoteli waliyofikia, jambo ambalo liliwakata stimu warembo hao.

 

“Walimaindi kweli, lakini ndiyo hivyo, hawakuwa na ujanja maana mtu chake,” kilisema chanzo chetu.

Mbaya zaidi, Sarah aliwakata maini warembo hao wa Kiganda baada ya kutupia ujumbe wa kumtakia Valentine’s Day njema mumewe huyo.

“Nakutakia Valentine njema…miaka minne tumekuwa pamoja,” aliandika Sarah kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hadi kwenye shoo, Sarah alikaba kwelikweli, hivyo kutowapa nafasi warembo wa Kiganda hata sekunde.

 

Hivi karibuni, meneja wa Harmo; Beauty Mmary ‘Mjerumani’ alizungumza na gazeti pacha la hili la IJUMAA na kudai kuwa wameamua kama uongozi msanii wao kutoambatana na mkewe katika kazi, lakini hata hivyo, inaonekana ‘kiapo’ hicho wamekivunja kimtindo.

KUFURU! UWOYA PESA INAONGEA, KODI YA MJENGO TU DOLA 1800..

Leave A Reply