Sasha afungukia video yake ya utupu

STAA wa filamu za Kibongo, Sasha Kassim, baada ya video yake ya utupu kuvuja kwenye mitandao ya kijamii akikata mauno hivi karibuni na kuibua maneno mengi, mwenyewe ameifungukia.  Akibonga na Shusha Pumzi, Sasha alisema video hiyo ni ya siku nyingi ambayo alimtumia mpenzi wake ambaye kwa sasa ameachana naye ndiye anaitumia kumchafua.

“Unajua hiyo video ni ya siku nyingi, kwa sasa nimebadilika na familia yangu inajua hivyo, wanaonichafua wana lengo lao baya, hata ukiiangalia na sasa nilivyo utabaini kuwa ni muda mrefu,” alisema Sasha.

Aliongeza kuwa, anashukuru si video ya mapenzi na kama ingekuwa hivyo angejiua kwani anaamini ndicho kitu ambacho kingemtia aibu. “Wee ingekuwa ya mapenzi ningejiua kwa sababu ni kitu ambacho naogopa sana na namuomba Mungu kisinitokee hata siku moja,” alisema Sasha.

STORI: HAMIDA HASSAN


Loading...

Toa comment