The House of Favourite Newspapers

SASHA AMCHONGEA KIBA KWA MKEWE

DAR ES SALAAM: Muuza sura (video queen) wa video za wasanii wa Bongo Fleva mwenye umbo matata, Sasha Kassim anadaiwa kumchongea staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ kwa mkewe, Aminah Khalef kwa kuanika meseji zao za faragha.  

 

Meseji hizo zilizovuja zilionekana kutoka kwa Kiba kwenda kwa Sasha usiku mnene, jambo ambalo ni hatari kwa jamaa huyo ambaye inasemekana mkewe alijifungua juzikati.

TUJIUNGE NA SHOSTI

Kwa mujibu wa mmoja wa mashosti wa Sasha ambaye jina lake linahifadhiwa, Sasha amekuwa na mawasiliano na msanii huyo hasa majira ya usiku. “Hivi mnajua kuwa Sasha ana mawasiliano na Kiba na kuna wakati anawasiliana naye mpaka usiku mwingi? “Kama hamuamini, mimi nitawaletea ushahidi wa chatting zao kwani nimezinasa kutoka kwenye simu ya Sasha mwenyewe, hata hivyo Sasha hamtaki Kiba, mkimbana nyinyi kwa njia zenu, atawaeleza ukweli,” alisema shosti huyo.

 

SMS ZAVUJA

Baada ya kutonywa kuwa kuna ushahidi wa meseji, Risasi Jumamosi lilifanikiwa kuzinasa SMS  hizo ambazo zilikuwa ni za kawaida, ingawa shosti huyo alidai kuwa kuna nyingine zinazoonesha jamaa huyo akimchombeza Sasha. “SMS nyingine siwapi, lakini muhimu nilitaka niwaambie tu kuwa hawa watu wanawasiliana na inaonesha kuwa jamaa anamhitaji Sasha,” alisema mvujishaji wa SMS hizo na kuongeza:

 

“Sasha hafuti meseji, anaweka tu simu yake hovyo sababu hamtaki Kiba, angekuwa anamtaka hata sisi isingekuwa rahisi kuziona, inaonekana kutokana na usumbufu anaoupata kutoka kwa Kiba yupo tayari mkewe ajue ili aache kumsumbua usiku.”

HUYU HAPA SASHA

Baada ya mazungumzo hayo, mwandishi wetu alimwendea hewani Sasha kwa njia ya WhatsApp na kumsomea mashitaka yake ambapo mwanzo alionekana kugwaya kuongea, lakini alipobanywa ‘kiufundi’, alikiri ‘kuimbishwa’ na Kiba na kwamba yeye hamtaki.

Risasi Jumamosi: Sasha hapa kuna SMS zako zimevuja unaonekana unaacha ovyo simu yako na marafiki  zako wanasoma meseji kama ambaye huhofii Kiba ameoa na mkewe akijua itakuwa msala.

 

Sasha: Sasa akijua kwanimimi najali? Sikia, mimi huyo Kiba simtaki yeye mwenyewe ndio ananisumbua. Tena kwa taarifa yako, sio Kiba tu hata wasanii wengine kibao wa Kibongo wananisumbua kweli siwataki, siwezi kutoka na msanii wa Bongo labda wa mantoni kama Chris Brown hivi.

Risasi Jumamosi: Kwa hiyo unataka kutuambia Kiba ndiye anayekusumbua na wewe humtaki hata kidogo?

Shasha: Ndio maana yake, pigia mstari.

MKE WA KIBA VIPI?

Jitihada za kumsaka mke wa Kiba ili kumsikia kama ubuyu huo wa motomoto umemfikia hazikuzaa matunda baada ya namba zake za simu kutopatikana kirahisi.

 

MAJIBU YA KIBA SASA

Baada ya kuzungumza na Sasha, Risasi Jumamosi lilimsaka Kiba kwa njia ya simu kisha akaelezwa jinsi Sasha ‘alivyomkaanga’ na kwamba yupo tayari meseji hizo zimfikie hata mkewe ili aache kumfuatilia, ambapo alipopatikana alijibu machache na kudai kuwa huwa hana mazoea ya kuchati na watu ovyo.

“Samahani sina tabia ya kuchati na watu ovyo,” alisema Kiba.Baada ya kimya cha muda mrefu, mapema wiki hii Kiba aliachia wimbo wake mpya wa Hela ambao baada ya muda aliufuta bila kutoa maelezo huku ikidaiwa kuwa ni kufuatia mashabiki wake kudai kuwa ni wimbo wake wa zamani.

STORI: HAMIDA HASSAN NA SHAMUMA AWADHI, RISASI JUMAMOSI

EXCLUSIVE: DIAMOND HAKUNIALIKA, ASIJISAHAU SANA – VIDEO

Comments are closed.