The House of Favourite Newspapers

Sauti Sol Watangaza Kutengana Baada ya Kuwa Pamoja kwa Miaka 20

0

KUNDI la muziki nchini Kenya, Sauti Sol linaloundwa na Mastaa wa kiume wanne kutoka Kenya, Bien-Aime Baraza, Willis Chimano, Polycarp Otieno na Savara Mudigi, limetangaza kutengana baada ya kuwa pamoja kwa Miaka 20

Kwa mujibu wa taarifa, Kundi hilo litatengana rasmi baada ya kumaliza ziara yao Desemba 16, 2023 na kila mmoja ataendelea kufanya shughuli zake binafsi ingawa urafiki na uhusiano wao hautavunjika

Wataanza ziara ya Kimataifa Mei 21, 2023 kwa kufanya matamasha 23 Ulaya na Marekani na kufunga ukurasa wao Jijini Nairobi Desemba 16, 2023. Hata hivyo, Mashabiki hawajafurahishwa na ratiba hiyo kutokuwa na Nchi za Afrika

#EXCLUSIVE: MAMA ALIYEOMBA NAMBA ya WAZIRI MKUU AANGUA KILIO KUKIMBIWA na MUMEWE, NAMJUA KAJALA…

Leave A Reply