The House of Favourite Newspapers

Sayansi Yasema: Binadamu hafi, hubadilika!

1

MAJENEZAYAJIDE.jpgMWandishi wetu, Amani

KWA zaidi ya miongo miwili sasa (miaka 10), wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je! Binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema hakuna kitu kama hicho.

Kuna wanasayansi wanaokiri kuwa, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, wana akili nyingi kuliko za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha, watoto hawa walianza kuzaliwa duniani mwaka 1975. Ni watoto ambao uelewa wao wa mambo ni mkubwa kuliko kawaida.

Baadhi ya watoto hao, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma kabla hawajafa. Wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao lakini wakaja kuzaliwa mahali pengine.

Hakuna idadi maalum ya watoto hao hapa duniani, lakini inadaiwa wako wengi. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wana kumbukumbu kali na uwezo mkubwa kiakili kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa ajabu.

KWA NINI WALIANZA KUZALIWA MWAKA 1975?

Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia kwa jumla. Kwamba, itafika mahali, maarifa yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kimekuja kumwonesha binadamu kuwa, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha ndivyo sivyo.

UTAFITI WA KARIBUNI

Hivi karibuni, mwanasayansi mmoja nchini India alikiri kuwa, binadamu akifa huenda kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine. Hii ina maana kuwa, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya tuliyonayo sasa.

Mwanasayansi huyo, Vikram Raj Singh Chauhan, alisema aliweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa miaka 6 ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh alisema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, akafariki dunia kwa ajali ya pikipiki.

Mtoto huyo akiwa na miaka miwili kwa sasa,  alisema kuhusu maisha yake ya nyuma kwamba alikuwa akitoroka sana nyumbani. Aliwaambia wazazi wake wa sasa kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyosoma.

Pia alikumbuka jina la baba yake wa zamani (kabla hajafa). Awali ilionekana kama amechanganyikiwa, lakini ilibidi wazazi wake wa sasa waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka umri.

SIKU YA KIFO CHAKE

Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa. Aliwaambia wazazi wake alifariki dunia,  Septemba 10, 1992 baada ya kugongwa na pikipiki akiwa kwenye baiskeli kwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo, alipata majeraha kichwani na alifariki dunia siku ya pili.

Baba yake wa sasa, Ranjit Singh, alisema mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, yeye na mkewe waliamua kumpeleka huko kijijini alikodai ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyo. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwataka waende kijiji cha jirani.

Kwenye kijiji hicho, walikwenda kwenye shule ambapo mwalimu mkuu alithibitisha kwamba, Septemba 10, 1992 kuna mwanafunzi alikufa kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shule hiyo, walibaini mahali wazazi wa awali wa mtoto huyo walipo.

Waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyo, Ranjit alieleza kuwa, mtoto wao aliwaambia madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu na alitaja kiwango cha fedha ambacho kilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.

Mama wa zamani wa mtoto huyo aliposikia hivyo aliangua kilio, kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye.

ARUDI KWA WAZAZI WAKE WA SASA

Baadaye, mtoto huyo aliondoka na wazazi wake wa sasa huku akiacha maswali yasiyo na majibu. Baadaye wazazi wake wa zamani na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwa wazazi wa sasa. Mtoto huyo aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.

Itaendelea wiki ijayo

1 Comment
  1. Manzi Salum says

    Hiyo sio,sayansi wala hakuna uvumbuzi kwani hilo linabebwa na Iman ya Mabaniani/Hindu ambao huamini muhindi akifa anachomwa moto kisha majivu hutupwa mto ghanga na hatimaye husafirisha kwenda baharini kisha wahindi kila pembe ya dunia huzaliwa.Akifa India atazaliwa amerika au Afika

Leave A Reply