The House of Favourite Newspapers

SBL, Club 1245 Waigeuza Jumapili kuwa Ijumaa Mpya

0

Ile Jumapili uliyoizoea ya kukaa kinyonge hatimaye imeondolewa kwenye kalenda, HAIPO TENA!

Wakali wa muda wote wa kutengeneza na kusambaza pombe kali na bia nchini hawa si wengine bali ni Serengeti Breweries Ltd wakishirikiana na club inayobamba mjini 1245 wameigeuza Jumapili yako kuwa Ijumaa mpya. Unaambiwa sasa siku za Jumapili zitakuwa maalamu za kula bata la babkubwa zikisindikizwa na burudani za kufa mtu, yote haya katika kuhakikisha kwamba unamalizia wikiendi yako vizuri kabisa tayari kwa kuanza wiki mpya.

SBL wanajulikana kwa utengenezaji na usambazaji wa pombe kali na bia zikiwemo Johnnie Walker, Guinness, Singleton, Gordons, Serengeti na nyingine nyingi. Sasa hapa vuta picha kolabo hili na club kali ya 1245 ambao nao ni wakali wa kuangusha bata zilizokwenda shule. Hakuna haja tena ya kusubiri Ijumaa, kwani hata Jumapili bado bata linaendelea Kulika tena katika ukali ule ule.

Andaa koo mapema kabisa, kwani Jumapili inayokuja ni mwendo wa bata bandika bandua ikiongozwa na Madj wakaili na burudani ya vinywaji vya kutosha. Kumbuka kuwa mtu makini kwa kutoendesha chombo cha usafiri ukiwa na kilevi kichwani.

Tupatane 1245 Jumapili hii!
#SBLx1245 #JumapiliKamaIjumaa #SpecialSuperSunday

Leave A Reply