The House of Favourite Newspapers

SBL yaahidi makubwa kuelekea mechi ya Stars na Equatorial Guinea

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Anitha Msangi(watatu kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wakutangaza maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea.

Mdhamini mkuu wa Timu yaTaifa (Taifa Stars) Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager,  imeahidi kuendelea kuwapa raha wapenzi wa soka hapa nchini kupitia udhamini wake kwa Timu yaTaifa. Taifa Stars,inatarajia kucheza mechi yake ya kufuzu tiketi ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea Novemba 15 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa TFF Kidau Wilfred (kulia), akiongea na waandishi wa habari kwenye mkutano huo.

Akizungumza wakati wa kutangaza maandalizi kuelekea mechi hiyo, Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi alisema SBL kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager ipo bega kwa bega naTimu ya Taifa pamoja na mashabiki wa soka.

“SBL kupitia bia yetu ya Serengeti Premium Lager tutataendelea kuwapa burudani mashabiki wa soka kwa kuhakikisha tunaiwezesha timu yetu ya taifa kufanya vizuri lakini pia kupitia bia ya Serengeti kuwa fanya mashabiki wafurahie mechi pamoja na bia yao pendwa,” alisema

Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji ya Taifa Stars Haji Manara (wapili kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mechi yake ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea

Anitha alisema, ilikuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanafurahia mechi hiyo, kampuni ya SBL itaweka skirini kubwa sehemu mbalimbali ambazo zitaonyesha mechi bure huku nafasi yakufurahia bia ya Serengeti ikitolewa.

“Tujitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu huku tukifurahia bia yetu ya Srengeti Premium Lager ambayo ni fahari yetu,” alisema Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kidau Wilfred alisema timu itaingia kambini hivi karibuni kujiandaa na mchezo huo wanyumbani..

Kidau alifafanua kuwa,mchezo wa pili wakufuzu AFCON utachezwa ugenini ambapo Stars watamenya na Libya Novemba 19,2019,siku 4 tu baada ya kucheza mchezo wa kwanza.

“Tunawaomba Watanzania kwa pamoja tuungane kwaajili ya timu yetu ya Taifa.Tujitokeze kwa wingi siku ya mechi na kuishangilia kwa nguvu zetu zote ilikuwapa hamasa wachezaji wetu waweze kufanya vizuri,” alisema Ndimbo.

Na Mwandishi Wetu

 

Comments are closed.