Scholes, Owen Hargreaves wampigia saluti Cavani

WACHAMBUZI wa soka, Paul Scholes na Owen Hargreaves wamempa sifa nyingi mshambuliaji Edinson Cavani mara baada ya kuonyesha uwezo wa juu katika ushindi wa Manchester United mabao 6-2 dhidi ya Roma, juzi Alhamisi.

 

Straika huyo raia wa Uruguay amefunga mabao mawili na kutoa asisti mbili katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford ikiwa ni nusu fainali ya kwanza ya Europa League.

 

Kwa matokeo hayo yanampa nafasi kubwa Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer nafasi kubwa ya kuingia fainali, ambapo timu hizo zinatarajiwa kurudiana wiki ijayo.

 

Scholes alisema: “Ilikuwa ni kazi kubwa ya mshambuliaji wa kati, tumekuwa tukiona wachezaji wengi wa timu hiyo Marcus (Rashford), Mason (Greenwood), (Anthony) Martial, wakiwa hawana uhakika kama wao ni washambuliaji wa kati au lakini wamepata jibu.

 

“Ameonyesha straika anatakiwa kucheza wapi na aliwafanya wenzake pia kucheza vizuri.” Upande wa Hargreaves naye aliongeza kuwa: “Nampenda Martial, nampenda Marcus (Rashford), lakini ni aina ya washambuliaji wa kisasa wanaoweza kucheza wakitokea pembeni.

 

Lakini Cavani ana uzoefu wa kucheza nafasi yake hiyo ya kati.”Katika mchezo huo United ilikuwa nyuma kwa mabao 2-1 hadi wakati wa mapumziko lakini ilirejea kwa nguvu na kufanya mashambulizi mfululizo yaliyowapa ushindi huo mnono.

MANCHESTER, EnglandTecno


Toa comment