Scholz Kansela Mpya wa Ujerumani , Aapishwa

Olaf Scholz ameapishwa kama Kansela mpya wa Ujerumani, na kuhitimisha miaka 16 ya kihistoria ya Angela Merkel kama kiongozi. Alipigiwa kura na bunge la Ujerumani, ambapo muungano wake wa vyama vitatu una wabunge wengi.

 

Wanademokrasia wake wa mrengo wa kati wa Social Democrats watatawala pamoja na Greens na Free Democrats-rafiki wa kibiashara. Kukabidhiwa madaraka kunaashiria mwisho wa maisha ya kisiasa ya Bi Merkel ya miaka 31.

 

Scholz, mwenye umri wa miaka 63, alikiongoza chama cha Social Democrats kupata ushindi wa uchaguzi mwishoni mwa Septemba, akijinadi kama mgombeaji wa kuendelea kwa sababu alikuwa na jukumu muhimu katika serikali ya Merkel kama makamu wa kansela.

 

Bunge la Ujerumani, Bundestag, liliunga mkono uteuzi wake kwa kura 395 dhidi ya 303, na kisha akateuliwa rasmi kama kansela wa tisa wa Ujerumani na Rais Frank-Walter Steinmeier.


Toa comment