Scrub ya sukari na mafuta ya mzaituni kwa midomo softi
Mwanamke mdomo bwana, tena mdomo wenye mvuto. Siyo mdomo umekauka, umepasuka utadhani sijui nini vile. Sasa basi, leo kwenye ukurasa huu nakuletea jinsi ya kulinda midomo yako isikauke na isipasuke kwa kutumia scrub ya sukari.
Hatua ya kwanza
Chukua sukari kiasi, changanya na mafuta ya mzaituni kiasi kwenye kibakuli mpaka yashikane.
Hatua ya pili
Chukua ule mchanganyiko wako, paka kwenye midomo kisha sugua taratibu kama unayefanya masaji kwa kutumia vidole na si mdomo kwa mdomo. Hii itasababisha kulainika kwa midomo na kuondoa ile ngozi iliyokauka.
Hatua ya tatu
Osha midomo yako kwa maji ya vuguvugu taratibu.
Hatua ya nne
Futa midomo yako kwa taulo laini kisha paka mafuta yako ya mdomo.
Unaweza kutumia mafuta yenye Aloe Vera au ya kawaida na utaona matokeo.
Nikuambie tu kwamba, kama una lile tatizo la kutoka ngozi ya mdomo kwa kufanya hivi utakuwa umelikabili.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!