Scrub ya sukari na mafuta ya mzaituni kwa midomo softi

zaiutuni, olivesMwanamke mdomo bwana, tena mdomo wenye mvuto. Siyo mdomo umekauka, umepasuka utadhani sijui nini vile. Sasa basi, leo kwenye ukurasa huu nakuletea jinsi ya kulinda midomo yako isikauke na isipasuke kwa kutumia scrub ya sukari.

Hatua ya kwanza

Chukua sukari kiasi, changanya na mafuta ya mzaituni kiasi kwenye kibakuli mpaka yashikane.

Hatua ya pili

Chukua ule mchanganyiko wako, paka kwenye midomo kisha sugua taratibu kama unayefanya masaji kwa kutumia vidole na si mdomo kwa mdomo. Hii itasababisha kulainika kwa midomo na kuondoa ile ngozi iliyokauka.

Hatua ya tatu

Osha midomo yako kwa maji ya vuguvugu taratibu.

Hatua ya nne

Futa midomo yako kwa taulo laini kisha paka mafuta yako ya mdomo.

Unaweza kutumia mafuta yenye Aloe Vera au ya kawaida na utaona matokeo.

Nikuambie tu kwamba, kama una lile tatizo la kutoka ngozi ya mdomo kwa kufanya hivi utakuwa umelikabili.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

globalbreakingnews.JPG


Loading...

Toa comment