visa

Sekeseke la Mastaa na Unga ni Fundisho

Wema Sepetu

NA ANDREW CARLOS |IJUMAA | SHOW-BIZ

ZIKIWA zimepita siku mbili tangu Mahakama ya Hak­imu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Sa­laam kuwaachia kwa dhama­na wasanii 13 kwa tuhuma za kutumia madawa ya kulevya, baada ya kuhenya chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi, sekeseke hilo ni vyema lika­chukuliwa kama fundisho kwao na wengine ambao hawajatajwa.

ILIKUWAJE?

Mwanzoni mwa mwezi huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ali­wataja wasaniii wa­naotuhumiwa kwa matumizi ya dawa hizo huku mastaa wengi wa Bongo Fleva na fil­amu wak­i w e m o kwenye l i s t i hiyo.

Mion­goni mwa wasanii hao ni Ha­midu Cham­buso (Dogo Hamidu au Nyandu Toz), Rajabu Salum (Mchafu Chakoma), Romeo Ban­gura (Rommy Jons), Cedou Madigo (Babuu wa Kitaa), Khalid Mo­hammed (T.I.D), Johana Mathysen (Director Jo­han), Winfrida Josephat (Recho Kizunguzungu) Anna Kimaro (Tunda), Wema Sepetu, Lulu Abbas (Lulu Diva) na Ahmed Hashim (Petit Man).

SEKESEKE KI­VIPI?

Ukiachana na kuta­jwa na kutakiwa kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi (Cen­tral), mastaa hao wal­itii amri hiyo lakini kitu kikubwa kwao ni sekeseke walilokutana nalo kuanzia siku ya kwanza walipotajwa na ku­kaa selo kwa zaidi ya siku tatu na wengine mbili.

Mastaa wengi walipotajwa majina yao na kutakiwa kufika kituoni hapo, walijua ni ishu ya kwenda kuhojiwa na kurudi lakini ikawa ndi­vyo sivyo kwani walijikuta wakiwekwa selo kwa siku hizo. Mbali na kuwekwa ndani huko, familia nyingi za wasanii hao zi­likuwa njia panda baada ya ndugu na watoto wao kuhusishwa na ma­tumizi hayo na pia kulazwa kituo cha polisi.

Tunda

Sekeseke lingine ni siku ya ku­fikishwa mahaka­mani am­bapo mastaa waliotuhumiwa wakiongozwa na TID, Nyandu Toz, Rommy, Mchafu na Babuu walikuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi kutokea central ambapo walipandishwa kwenye ‘difenda’ ya polisi na hata wal­ipofikishwa nje ya mahakama walipangish­wa foleni ya kuchuchumaa mmoja mmoja.

Walionekana kutokuwa na furaha, sura zao zilikuwa za huzuni na kuwafanya hata ndugu zao nao kuwaonea huruma. Ilikuwa ni fedheha kwao hasa ukichukulia ile hadhi waliyokuwa nayo huko mtaani kama mastaa la­kini pia kile wali­chotuhumiwa nacho.

Recho

Yawezekana wapo wanao­jutia kwa kuwa wanatuhumiwa kwa kitu ambacho kweli wanakifanya. Kama ni hivyo, basi kujuta huko kuwe sababu ya wao kubadilika.

Ukijaribu kufuatilia kwa karibu utagundua kuwa nia ya Mhesh­imiwa Makonda haikuwa mbaya, alifanya vile katika jitihada za kupambana na tatizo hilo ambalo limekuwa ni tisho katika jamii yetu.

TID

Lakini pia baadhi ya waliokuwa na msala huo waliwahi kutuhu­miwa huko nyuma lakini walikuwa wakikana wakisema wanasingizi­wa. Kwa hapa walipofikia ni vyema kwa kile kilichowapata kikawa ni fundisho kwao na wanachotakiwa kufanya ni kubadilika tu.

Inafahamika kwamba, kujihusi­sha kwa namna yoyote na mambo ya madawa ya kulevya ni kosa kish­eria ambalo linaweza kukuharibia maisha yako, sasa kama wewe ni msanii mwenye future yako, kwa nini ujiingize huko? Hujitaki?

Rommy Jons

Labda niseme tu kwamba, wa­liotuhumiwa kwenye soo hilo la unga wanatakiwa kuchukua hat­ua za haraka za ‘kuyapaka rangi’ majina yao badala ya kuendelea kuyachafua. Pia iwe fundisho kwa wengine ambao wanatumia, wa­nauza au kusafirisha lakini kwenye awamu hii hawakutajwa. Huenda siku wakitajwa wakahenyeka zaidi ya wenzao waliotangulia.

Petit Man

Hili lisiwe kwa mastaa tu, hata wengine wanaojihusisha na madawa ya kulevya ni vyema wakachukulia hiki kilichowapata mastaa hao kama fundisho kwao. Ni imani yangu kwamba, kwa joto ya jiwe walilopata mastaa hao itakuwa ni chachu ya mabadiliko kwa jamii nzima.

WALIPO MASTAA HAO

Kwa sasa baadhi ya mastaa hao wakiongozwa na TID na Tunda wapo nje kwa dhamana baada ya mahakama kutoa uamuzi wa kuwa chini ya uangalizi kwa kipin­di cha mwaka mmoja kwa mujibu wa kifungu cha 73 (e) na 74 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na kujidhamini wenyewe kwa dhamana ya Sh. Milioni 10 kila mmoja pamoja na kuripoti Central Polisi kwa mwezi mara mbili.

Save

Save

Save
Toa comment