The House of Favourite Newspapers

Sekeseke… Wapinzani Wagomea Kuapishwa Mbunge wa CUF ya Lipumba (Video)

0
Picha na maktaba.

SEKESEKE Party Two limeuibuka tena bungeni Dodoma leo Septemba12, 2017 mara baada ya wabunge wa Chama Cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kugomea kuapishwa kwa mbunge Rehema Juma Migila wa chama hicho.

Katika sekeseke hilo, wabunge wa upinzani CUF na wale wa Chadema, walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kumwapisha mbunge huyo ambaye ni miongoni mwa wabunge nane walioteuliwa hivi karibuni na Tume ya Uchaguzi baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambulika na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba kuwavua uanachama wakati Spika Ndugai akiwavua ubunge.

Wiki iliyopita wabunge hao waligomea kuapishwa kwa wabunge saba wa CUF walioteuliwa na NEC huku wakieleza kuwa hawatambui wabunge hao wapya wa CUF.

Leave A Reply