Sekondari ya St.Mark’s Yajivunia Maadili ya Wahitimu Wao

Mmoja wa wahitimu akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi.

Uongozi wa Shule ya Sekondari  St.Mark’s iliyopo Kongowe Jijini Dar es Salaam kuwajenga kimaadili wanafunzi wao kumesaidia mpaka sasa takribani miaka 17 na kusababisha mtoto hata mmoja kutokuacha shule kwa kupata mimba za utotoni.

Akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne mkurugenzi wa shule hiyo, Peter Mutembei amesema kuwa maadili ambayo yametolewa katika shule hiyo yamewajenga watoto uwezo kutojishughulisha na mambo ya siyofaa.

“Walimu ni walezi wakubwa wa watoto na wanakuwa nao karibu na kushinda nao muda mrefu shuleni pia walimu wanafahamu zaidi tabia za wanafunzi hivyo wanalazimika kuwapatia maadili ili wote wawe kitu kimoja.” Amesema Mutembei.

Ameongeza kuwa maadili hayo, yamesaidia ambapo mpaka sasa shule ina  miaka 17 hakujawahi kutokea mtoto kapata mimba maadili ambayo yanatolewa kwa  wanafunzi wao na wamekuwa wakiwasisitiza hata wakirudi nyumbani wayaendeleze.

Nae Mkuu wa shule hiyo, Leticia Joseph amesema wanaipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kumtanguliza Mungu kwa kuandaa utaratibu wa maombi katika kipindi cha corona ambapo maombi yalifanyika na kusaidia kupotea kwa ugonjwa huo.

Sehemu ya wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.

“Tunaishukuru Serikali iliruhusu masomo yaendelee huku kukiwa  na corona pamoja na ruhusa  hiyo iliendelea  kutolewa  elimu ya kujikinga na ugonjwa huo, ambapo ilisaidia hakuna mtoto hata mmoja aliyekufa na ugonjwa huo.”Amesema Mwalimu Leticia.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Neema Magembe ambaye ni Afisa Elimu Sekondari, Temeke amesema kuwa serikali inataka kila mtoto aliye na sifa ya kusoma apelekwe shule.

“Serikali imekuwa ikitoa kila mwezi  kiasi cha shilingi bilioni 300 kwa ajili ya kupelekwa katika elimu.

Ninawataka wahitimu walio na sifa za kupiga kura wajitokeze na wachague viongozi kutokana na sera zao.”Alimaliza kusema.

Toa comment