The House of Favourite Newspapers

Sekretari wa Manji Amtetea Bosi Wake Mahakamani

0
dawa za kulevya
Yusufu Manjia akiteta na mawakili wake mahakamani.

 

KESI ya dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji, imeendelea leo wakati wa kusikiliza ushahidi ambapo umetolewa na mtu wa tatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, shahidi wa kwanza alikuwa ni Maria Rugalabumu ambaye amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba yeye ni sektretari wa Manji (katibu muhtasi) kutoka ofisi ya Quality Group Ltd ya jijini Dar es Salaam.
Wakati wa kusikiliza ushahidi wake alikuwa akiongozwa na wakili wa utetezi, Hajra Mungula, ambapo amedai alianza kufanya kazi katika kampuni hiyo tangu miaka 1990 wakati Manji akiwa bado anasoma shule baada ya kurithi mikoba ya baba yake.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya vitu anavyomhifadhia Yusuf Manji alisema kuwa vipo kutokana na jinsi bosi wake anavyomwamini.

 

Rugalabamu amedai kuwa anashangazwa kusikia kuwa Manji anatumia dawa za kulevya jambo ambalo si kweli kwani amemfahamu takribani akiwa bado mdogo.

Alitaja pia kwamba majukumu yake ni uangalizi wa ofisi yake ikiwemo kuchapa barua, kupokea wageni na kutuma barua zinazotoka ofisi yao na alimsifia bosi wake kwa utendaji kazi wake wa kazi za kila siku.

 

Vilevile ameieleza Mahakama kwamba yeye ndiye aliyetoa kopi ya nakala ya dawa za Manji kutoka kwa daktari wake aliyeko Marekani wakati Manji alipokuwa rumande.

\
Ameeleza kwamba nakala hiyo aliipata kwa njia ya barua pepe (e-mail) ambapo baada ya kuitoa nakala alimpatia askari ili ampe Manji ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, hivyo aliiomba Mahakama ipokee hati hiyo kama sehemu ya kielelezo.

Naye Wakili wa Serikali, Timony Vitalis, alipinga kupokelewa kwa hati hiyo kwa sababu haina uthibitisho wa kiuhalisia na daktari aliyeituma.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Mkeha alitoa uamuzi ambapo alikubaliana na Wakili Vitalis, akisema Mahakama haiwezi kupokea kielelezo hicho.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply