The House of Favourite Newspapers

Sekta Binafsi Yaipongeza Serikali kwa Mazingira Rafiki ya Biashara

0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Godfrey Simbeye.

TAASISI ya sekta binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) imeipongeza serikali kwa kuendelea kuweka mazingira ya kuboresha biashara nchini.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, taasisi hiyo imeeleza kuwa hivi karibuni sekta binafsi imekuwa ikifanya majadiliano baina yake na sekta ya umma katika ngazi za wizara, mikoa hadi wilaya.

Katika taarifa hiyo pia imesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuongoza Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) linalotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu.

Taarifa hiyo pia imekumbusha kwamba Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) liliundwa kupitia waraka wa Rais mwaka 2001 ambapo madhumuni yake ni majadiliano ma mwelekeo kuhusu masuala ya kimkakati yanayohusu mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Imeelezwa kuwa TNBC ndiyo jukwaa kubwa kwenye masuala ya majadiliano baina ya serikali na sekta binafsi ambapo baraza hilo huundwa na wawakilishi 20 kutoka serikalini ambao ni mawaziri, Gavana wa Benki Kuu na Mwanasheria Mkuu ambapo kwa upande wa sekta binafsi nayo hutoa wawakilishi 20 na kupendekeza ajenda ya kikao.

Taarifa hiyo imekumusha kwamba mnamo Desemba 2015 baada ya Rais Magufuli kuapishwa, alikutana na sekta binafsi na kufanya mazungumzo na wahusika ambapo aliahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jumuiya ya wafanyabiashara na sekta binafsi nchini kuonyesha alikuwa na nia madhubuti ya kuendeleza sekta binafsi na kukuza uchumi nchini.

Stori: Denis Mtima/GPL

Leave A Reply