The House of Favourite Newspapers

Senzo ampiga stop Sven

0

Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, amepiga mkwara kwamba kikosi hicho kinachoongozwa na kocha Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, kwa sasa hakitakiwi kupoteza pointi yoyote kwenye mechi yao ya ligi mara baada ya kufungwa katika mechi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania.

 

Senzo, raia wa Afrika Kusini, ameweka wazi hilo kwamba wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kupambana kuona hawapotezi pointi yoyote katika michezo yao 18 iliyobakia ya Ligi Kuu Bara.

 

Hadi sasa Simba katika mechi zake 20 za ligi, imepoteza mbili dhidi ya Mwadui na JKT Tanzania, ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 50.

 

Senzo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa kwa sasa hawatakiwi kupoteza pointi tena baada ya kuzikosa pointi tatu mbele ya JKT Tanzania ambapo wanatakiwa kupambana kupata matokeo mazuri katika mechi zao 18 zijazo.

 

“Kwa sasa hatutakiwi kupoteza pointi tena baada ya kufungwa mechi iliyopita, tunatakiwa kuchukua pointi katika kila mchezo wetu unaokuja.

 

“Tuna mechi 18 zijazo zote hizo tunatakiwa kupambana kupata matokeo mazuri kwa sababu tumeona jinsi hali inavyokuwa mbaya wakati ambao tunapoteza mechi kama ilivyokuwa mara ya mwisho na JKT,” alisema Msauzi huyo.

Said Ally, Dar es Salaam MTENDAJI

Leave A Reply