The House of Favourite Newspapers

Senzo Ataja Sababu ya Kumpa Ukocha Nizar

0

MSHAURI Mkuu wa Klabu ya Yanga kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko, Senzo Mazingisa amesema kuwa wameamua kuwaongeza vijana ndani ya timu ili kwenda na kasi ya soka la kisasa.

 

Yanga, juzi Januari 27 ilimtambulisha Nizar Khalifan kuwa kocha msaidizi akichukua mikoba ya Juma Mwambusi ambaye aliomba kujiweka kando kutokana na matatizo ya kiafya pamoja na Edem Mortotsi kuwa kocha wa viungo.

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

Nizar alikuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya African Lyon ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na pia aliwahi kucheza timu ya Mtibwa Sugar pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mazingisa alisema: “Tunahitaji kuongeza thamani ya ubora katika benchi ndiyo maana wote ni vijana na hata kocha mkuu wetu ni kijana ili kuendana na soka la kisasa.

”Aliongeza kuwa anaamini watu waliochaguliwa ni sahihi na watafanya kazi kwa ushirikiano kufanikisha malengo waliyojiwekea katika msimu huu.“

 

Ninaona watu ambao wamechaguliwa ni watu wazuri, hivyo ni suala la kusubiri na kuona namna ambavyo tutaendelea kupambana,” alisema Senzo.Yanga inashika nafasi ya kwanza katika ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza michezo 18.

Stori: Wilbert Molandi,Dar es Salaam

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply