The House of Favourite Newspapers

SEPTEMBA CHUNGU KWA MASTAA HAWA

Image result for soudy brown na maua sama

FEBRUARI, mwaka jana, ilikuwa chungu kwa mastaa wengi wa filamu na Bongo Fleva baada ya kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusika katika matumizi ya dawa za kulevya.

Mastaa hao waliotajwa ni Wema Isaac Sepetu, Agness Gerald ‘Masogange’ (sasa marehemu), Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, Khaleed Mohamed ‘TID’, Ahmed Manunge ‘Petit Man’, Winfrida Josephat ‘Recho’ na wengine wengi ambao kwao mwezi huo ulikuwa mchungu hasa baada ya kutakiwa kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar.

Tangu ishu hiyo itokee ambayo iliwafikisha baadhi yao mahakamani na kuchukuliwa hatua, hakukuwa na sakata kubwa lililowasababisha mastaa wengi kusota lupango. Septemba, mwaka huu, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya mastaa kujikuta wakisota lupango kwa sababu tofauti na katika makala haya, yanawaanika mastaa hao;

SOUD BROWN NA MAUA SAMA

Septemba 16, mwaka huu ilikuwa kama utani baada ya tetesi kusambaa kuwa mtangazaji wa ‘Shilawadu’, Soudy Brown na staa wa Bongo Fleva, Maua Sama wamekamatwa na Polisi wakidaiwa kudhalilisha Nembo ya Taifa kwa kuchezea fedha za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye kuwa kweli. Wakati wakiwa mahabusu, Soudy alipata msala mwingine wa kudaiwa kutumia maudhui ya mtandao bila kuwa na kibali.

Msala uliowagusa wote wawili ni ule wa kurusha kipande cha video kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kinachoonesha watu wasiofahamika, wakicheza wimbo wa Maua uitwao Iokote huku wakirusha noti za elfu kumi juu na kuzikanyaga.

Awali, wawili hao walitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kisha wakapelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, wakawekwa ndani wakati jeshi hilo lilipoanza uchunguzi wake.

Hata hivyo, jeshi hilo liliendelea na uchunguzi wake kwa takriban siku 7 na ilipofika siku ya 8 (Septemba 24, mwaka huu), Soudy pekee ndiye aliyepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu jijini Dar. Kwa sasa wawili hao wapo nje kwa dhamana.Image result for shaffih dauda

SHAFFIH DAUDA

Wakati sakata la Soudy Brown na Maua Sama likiendelea kuwa moto, ishu nyingine ikaibuka, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikidaiwa kuwashikilia mtangazaji wa Clouds, Shaffih Dauda na MC Luvanda kwa kile kinachodaiwa kumiliki Mitandao ya Youtube bila kusajili maudhui.Image result for sister fay holly star

SISTER FEY, HOLLY STAR

Septemba 19, haikuwa nzuri kwa msanii wa Bongo Fleva, Faidha Omary ‘Sister Fey’ na mpenzi wake, Elias John ‘Holly Star’ baada ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa kosa la kukiuka maadili kwa kuchapisha maudhui yanayodhalilisha kwenye mitandao ya kijamii kwa amri ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Katika taarifa ya Juliana Shonza, aliiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kumfuatilia Sister Fey juu ya matumizi yake ya mitandao na mwishowe waliwakamata usiku na kuwaweka Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) jijini Dar ambapo kwa sasa wanasubiriwa kupandishwa mahakamani.Image result for uwoya na tausi

UWOYA, TAUSI…

Hii ilikuwa usiku wa Septemba 22, mwaka huu ambapo mastaa kadhaa wa Bongo Movies, Irene Uwoya, Tausi Mgedela, Idris Makupa ‘Kupa’, Hamis Changale ‘Mtanga’ na wengineo walikamatwa na Polisi wa doria jijini Mbeya kwa kosa la kunywa pombe wakiwa wamevuka muda wa baa kufungwa.

Uwoya na wenzake hao walikutwa na kisanga hicho walipokwenda kwenye tamasha maalum la Mimi Nimefurahi ambapo baada ya shughuli hiyo ndipo wakazama kwenye baa hiyo kupoza koo na mashabiki wao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, walifanya hivyo kwa sababu wao ni kioo cha jamii hivyo wawe mfano.

STORI: ANDREW CARLOS

Comments are closed.