SERENGETI BOYS U17 YACHAPWA 5-4 NA NIGERIA TAIFA

Kikosi cha timu ya Serengeti Boy U 17 kilichoanza dhidi ya Nigeria.

 

WENYEJI, Tanzania wameanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) baada ya kuchapwa mabao 5-4 na Nigeria katika mchezo wa ufunguzi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya leo.

Sasa kikosi cha kocha Oscar Rabson Mirambo kina kazi ya kuupanda kuhakikisha kinashinda mechi zake mbili zijazo dhidi ya Angola na Uganda ili kuwania tiketi ya Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini Brazil.

Kikosi cha timu ya Nigeria.

Hadi mapumziko, Nigeria inayofundishwa na kocha mzalendo pia, Manu Garba ilikuwa mbele kwa mabao 3-1.

Mabao ya Tanzania yamefungwa na Edmund 22′ (P) 60′, Kelvin 52′ na  Maurice 57′ (P)  kwa upande wa Nigeria yamefungwa na Olatomi 21′, Ubani 30′ 72′, Amoo 36′ na Ibraheem


Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Mwinyi Yahya, Arafat Swakali, Mustapha Nankuku, Alphonce Msanga, Misungwi Chananja/Edson Mshirakandi dk34, Edmund John, Kelvin John, Pascal Msindo, Dominic William, Ally Rutibinga na Morice Abraham/Ladaki Chasambi dk82.


Nigeria; Suleman Shaibu, Shedrack Tanko, Ogaga David Oduko, Samson Tijani, Clement Ferdinard Ikenna, David Ishaya, Olakunle Olusegun, Mayowa Abayomi/Fawaz Abdullahi dk80, Wisdom Onyedikachi Ubani, Akinkunmi Amoo na Olatomi Olaniyan/Ibraheem Jabaar dk71.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Loading...

Toa comment