The House of Favourite Newspapers

Serikali Yatoa wito kwa NBC kupanua wigo katika utoaji wa huduma zake

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Theobald Sabi  akimkabidhi Waziri Mkuu hundi yenye thamani ya shilingi 11,270,00 zitakazosaidia katika ujenzi wa kituo cha polisi wilani Ruangwa.

 

SERIKALI imetoa wito kwa Benki ya Biashara nchini NBC kupanua wigo katika utoaji wa huduma zake hapa nchini ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuhifadhi fedha zao katika eneo salama.

 

Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi ofisini kwake  jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema wakati serikali ikiendelea kuhamasisha wananchi kuongeza nguvu katika sekta ya kilimo, taasisi za fedha hazinabudi kusogeza huduma zao karibu na wanchi ili waweze kutunza fedha zao katika hali ya usalama badala ya kuhifadhi majumbani.

 

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa  ameipongeza benki  ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwawezesha wananchi kupitia mikopo kwa wajisriamali wadogo ambayo inawawezesha kuongeza mitaji yao ya biashara mbalimbali.

 

Katika hatua nyengine Mkurugenzi  huyo wa NBC amemkabidhi Waziri Mkuu hundi yenye thamani ya shilingi 11,270,00 zitakazosaidia katika ujenzi wa kituo cha polisi wilani Ruangwa.

Comments are closed.