Serikali Inatambua Umuhimu Wa Kukuza Usawa Wa Kijinsia Na Uwezeshaji Wanawake – Majaliwa
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini, yanayofanyika katika viwanja vya Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama njia mojawapo ya kuimarisha ustawi na kufikia maendeleo jumuishi na endelevu.