The House of Favourite Newspapers

Serikali kubadili sera ya maendeleo, utamaduni

0

1

Mkurugenzi Msaidizi wa Lugha katika Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Hajjat Kitogo, akisoma taarifa.

2.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Leah Kihimbi (kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo baada ya kupokea maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).

3

Viongozi hao wakiandika maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari.

4

Wanahabari wakichukua matukio katika mkutano huo.

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Idara ya Maendeleo na Utamaduni inatarajia kuja na mabadiliko mapya ya sera ya mwaka 2016 badala ya ile ya zamani ya mwaka 1997 ambapo wadau mbalimbali wameshirikishwa kutoa maoni yao ili yatumike kuboresha sera hiyo.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Lugha Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Hajjat Kitogo, amesema kuwa rasimu ya sera hiyo ya mwaka 2016 imekwishakamilika na tayari inapatikana katika tovuti ya wizara ambayo ni www.habari.go.tz.
Pia aliongeza kuwa, kwa wale wanaotaka kutoa maoni yao wanaweza kupitia tovuti ya wananchi ambayo ni www.wananchi.go.tz hata kupeleka kwa njia ya maandishi ya mkono.
Aidha Kitogo alibainisha maeneo makuu 13 ambayo mtu akitoa maoni yake yatakuwa yamelengwa ambapo baadhi ya maeneo hayo ni kuwa na jamii inayothamini na kuenzi maadili, mila na desturi, kukuza na kuendeleza matumizi sanifu na fasaha ya lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa, kuwa na kazi za sanaa zenye ubora unaokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa pamoja na kuwa na utaratibu endelevu wa kukusanya, kuorodhesha, kuhifadhi, na kusambaza tafiti za sekta ya utamaduni na sanaa.

Na Denis Mtima/Gpl

Leave A Reply