Serikali Kujenga Chato Stadium ya Ukweli – Video

SERIKALI imesema imedhamiria kujenga uwanja mkubwa wa mpira wa miguu wilayani Chato, mkoani Geita ambako ni nyumbani kwa Rais John Magufuli, ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji.

 

Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo leo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

“Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu,” amesema Kalemani.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMA


Loading...

Toa comment