Serikali Kupokea Dozi Mi. 2 za Uviko Kutoka China

MSEMAJI mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema mwanzoni mwa mwezi ujao serikali itapokea dozi milioni 2, za kujikinga na ugonjwa wa Uviko-19 kutoka nchini China, Msigwa ameyasema hayo leo Septemba 25, wakati akitoa taarif ya wiki ya Serikali mkoani Singida.

 

 

“Tunatarajia mwanzoni mwa mwezi ujao chanjo nyingine dozi Milioni 2 kutoka nchini China (SINOPHARM) zitafika nchini ili Watanzania waendelee kupata chanjo bila matatizo”

 

“Kwa kutambua kuwa chanjo zinaweza kuisha muda wowote kuanzia sasa, Serikali inakamilisha utaratibu wa kuleta chanjo nyingine dozi Milioni 2 kutoka nchini China (SINOPHARM) “ameongeza Msigwa

 

 

Msigwa pia amewasihi wale ambao hawependi kuchoma sindano kuchangamkia dozi ya Janssen ambayo unachoma mara moja tu.

 

“Nawasihi wale ambao hawapendi kuchoma sindano mara mbili kuchoma chanjo zilizopo sasa kabla hazijaisha kwa sababu chanjo zinazotolewa sasa ni aina ya JANSSEN (JJ) kutoka Marekani, chanjo hizi unachoma mara moja tu na unapata kinga ya mwaka mzima”.


Toa comment