The House of Favourite Newspapers

Serikali Kuunda Chombo Maalum Kushughulikia Tatizo la Afya ya Akili – Video

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya wabunge, wakati wa kikao cha tatu cha Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge, bungeni jijini Dodoma, Oktoba 31, 2024.

Serikali imesema imeanza mchakato wa utungaji wa sheria ya kuanzishwa kwa Baraza la Afya ya Akili, ili lianze kufanya kazi na utakapokamilika mpango kazi na utekelezaji utawekwa wazi.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika maswali ya hapo kwa papo bungeni mkoani Dodoma, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu aliyehoji sababu za kutokamilika kwa mchakato wa kuundwa kwa baraza hilo.

Bara la Afya ya Akili litakuwa na majukumu ya kusimamia muundo wa kuratibu sekta za kitaaluma na kiutendaji kushughulikia ufanisi wa suala la afya ya akili nchini na kutengeneza skimu kwa ajili ya kuajiri wataalam watakaosimamia jambo hilo.