The House of Favourite Newspapers

Serikali nchini kenya yaagiza shule zote zifungwe

0

Mgomo-Kenya
Serikali ya nchini Kenya imeagiza shule zote zifungwe kuanzia Jumatatu kufuatia mgomo wa walimu unaoendelea nchini humo.

150114152629_wanafunzi__640x360_bbc_nocreditWizara ya elimu nchini humo, imetoa barua kwa shule zote za umma na za kibinafsi ikiagiza zifungwe na wanafunzi warudi majumbani kwao.

Aidha serikali imesema kuwa, watakabakia shuleni pekee,  ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.

Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini Kenya (KNUT) amesema kuwa, tayari amepokea barua hiyo yenye agizo la serikali kuhusu kufungwa kwa shule zote nchini humo.

Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule “zamani”.

Inujaa ijayo, mahakama nchini Kenya inatarajiwa kuamua iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali au la.

Leave A Reply