The House of Favourite Newspapers

Serikali: Tuwe Wazalendo, Tuisapoti Stars

0

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, amewataka Watanzania wote kuwa wazalendo na kutoa sapoti ya kutosha kwa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

 

Waziri Bashungwa aliyasema hayo jana Jumamosi katika mkutano maalum na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Waziri Bashungwa alisema: “Kwanza napenda kumshukuru Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kuniamini na kunipatia wajibu wa kuiongoza wizara hii, lakini niwashukuru pia wahusika wote wa vyombo vya habari kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya ya kuuhabarisha umma wa Watanzania.

“Lakini kama Watanzania bado tuna deni kubwa sana la kuendelea kuwa wazalendo, na kuisapoti timu yetu ya Taifa kwani kwa kufanya hivyo tutawapa vijana wetu nguvu ya kupambana zaidi kupata mafanikio, na mafanikio hayo ni kitu cha kujivunia kwa kila Mtanzania.”

 

Kwa sasa Stars ipo kambini ikijiandaa na michuano ya CHAN itakayofanyika hivi karibuni nchini Cameroon. Kuelekea michuano hiyo, keshokutwa Jumanne, Stars itacheza mchezo wa kirafi ki dhidi ya DR Congo.

JOEL THOMAS NA SAID ALLY,Dar es Salaam

Leave A Reply