The House of Favourite Newspapers

Serikali ya CCM yaahidi kuweka umeme vijiji vyote tanzania ndani ya miaka miwili

0

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga. Miongoni mwa ahadi aliyoitoa kwa wanaKilindi ni kulishughulikia suala la upatikanaji wa huduma za maji safi na salama pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka katika Wilaya hiyo.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano mdogo wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Kilindi, Tanga.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto. Baadhi ya ahadi aliyoitoa Bi. Samia ni pamoja na upimaji wa ardhi ya vijiji na wilaya ili kumaliza migogoro ya ardhi kwa wafugaji na wakulima.

 

Leave A Reply