The House of Favourite Newspapers

Serikali yakamata Mali za bilionea wa unga

0

DSC_0121

Akiwa mikononi mwa polisi.

Mwandishi wetu

KUMEKUCHA! Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amewasilisha waraka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akitaka kushikiliwa na kuzuiwa kwa mali zote za mtuhumiwa wa madawa ya kulevya ‘unga, Muharami Abdallah au maarufu kwa jina la ‘Chonji’ na mkewe, Mwalibora Nyanguri kuhamisha umiliki, kupangisha au kuombea mikopo.

IMG_1239

Vitendea kazi alivyokutwa navyo.

Maombi hayo dhidi ya Chonji na mkewe yaliwasilishwa kwa hati ya dharura mahakamani hapo Septemba 13, mwaka huu mbele ya Jaji Wilfred Dyansobela.

MBALI YA CHONJI  NA MKEWE
AG ameiomba mahakama hiyo imzuie Chonji, mawakala wake au mtu mwingine yeyote kwa niaba yake, kuhamisha umiliki wa mali, kupangisha nyumba au kuombea mikopo (ili serikali ifuatilie uhalali wa upatikanaji wa mali hizo).

IMG_1280

Mjengo anaomiliki.

MALI ZENYEWE
Mahakama hiyo imetakiwa kutoa zuio hilo kwa nyumba sita za Chonji zilizopo maeneo ya Magomeni, Tandale Ziota na Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.

Nyumba hizo ni namba 95280 iliyopo Kiwanja Namba 43 Kitalu O, Namba 90292 iliyopo Kiwanja Namba 66 Kitalu P, nyumba iliyopo Kiwanja Namba 68 Kitalu X, nyumba yenye Mita ya Luku Namba 43001304757 na nyumba nyingine yenye Mita ya Luku Namba 04215118664.

MPAKA MAGARI
Mali nyingine zilizowekewa zuio na kuwa chini ya serikali ni gari aina ya Mitsubishi Canter yenye namba za usajili T 376 BYY, Toyota Verossa yenye namba za usajili T 326 BXF na mali nyingine zote zenye jina au umiliki wa Kampuni ya Mumask Investment ambayo ipo chini ya mtuhumiwa huyo.

DSC_0097MAAGIZO MPAKA WILAYANI
Katika maombi hayo, AG amemwomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na Ofisa Mtendaji wa Mtaa (husika) wasipitishe uhamishaji wa umiliki wa nyumba hizo na mahakama imwamuru Msajili wa Ardhi kutambua kwamba nyumba hizo zimewekewa pingamizi.

Maombi hayo kwa mara ya kwanza yalitajwa katika mahakama hiyo Novemba 12, mwaka huu ambapo mahakama iliamuru wadaiwa kuwasilisha hati kinzani Novemba 26 (leo) na AG atajibu Desemba 3, mwaka huu na maombi yatasikilizwa Desemba 4, mwaka huu.

KISA CHA YOTE HAYA
Chonji anakabiliwa na kesi ya jinai namba 50 ya mwaka 2014 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ambapo anatuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi 227, 374,500. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi, Janet Kaluyenda.

Hata hivyo, katika Mahakama ya Kisutu kesi hiyo ilitajwa jana Novemba 25. Mtuhumiwa huyo anapelekwa mahakamani akitokea katika Gereza la Keko jijini Dar.

AHADI YA RAIS MAGUFULI
Akilifungua bunge mjini Dodoma, Ijumaa iliyopita, Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ alisema amedhamiria kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya ambapo alisema atashughulika zaidi na vigogo (wauzaji) badala ya vidagaadagaa (watumiaji) huku akisema kazi hiyo na ile ya kupambana na mafisadi ni sawa na kutumbua jipu na kujipambanua kuwa, anataka kuwa mtumbua majipu huku akitaka kusaidiwa na idara husika za kupambana na mambo hayo!

Leave A Reply