Serikali Yaondoa Zuio la Uchimbaji wa Mawe Unguja, Mkuu wa Mkoa Afunguka
Mkuu wa Mkoa wa Unguja Kaskazini, Ayoub Mahmoud amesema serikali kupitia sekta ya nishati na madini imefanya uamuzi wa kuruhusu uchimbaji wa mawe katika eneo la Bubwini, Makoba na Mafufuni ambao ulipigwa marufuku mara baada ya kusababisha madhara mbalimbali hapo awali.
Akizungumza na Global Tv baada ya kufanya ziara yake katika maeneo hayo, Mkuu wa Mkoa amesema kutokana na wananchi wa eneo hilo kutegemea shughuli ya uchimbaji wa mawe kama sehemu ya kujiingizia kipato serikali imeona ipo haja ya kuruhusu shughuli hiyo kwa utaratibu maalumu bila kuleta madhara ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo machache yatakayoweza kutimika kwa kazi hiyo.
“Moja ya shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Bubwini ni uchimbaji wa mawe ambao kwasasa serikali kupitia sekta ya nishati na madini wamefanya maamuzi ya kuruhusu uchimbaji huo na kutenga maeneo machache yatakayoweza kutumika kwa shughuli hiyo.
Aidha ameeleza kuwa wananchi wa Bubwini wanategemea zaidi shughuli za kilimo, uvuvi pamoja na shughuli za uchimbaji wa mawe ambapo mara baada ya kutolewa kwa tamko la zuio la uchimbaji wa mawe liliwapa mshituko mkubwa wananchi hao wakihofia kuyumba kiuchumi.
SHIGONGO AUMA MENO kwa HASIRA – “MOTO UTAWAKA HAPA LEO KAMA HIKI KIPENGELE HAKITABADILIKA”…