The House of Favourite Newspapers

Serikali Yaruhusu Mashabiki Kuingia Mechi Ya Prisons Na Simba

0

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imepokea ombi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya la kuruhusiwa kuingiza washangiliaji katika Michezo ya nyumbani ya klabu ya Prisons FC.

 

Katika ombi lake Mkoa wa Mbeya umeelezea mpango mkakati wa kutekeleza na kusimamia kikamilifu Mwongozo wa afya michezoni katika kipindi hiki cha tahadhari ya maumbikizi ya ugonjwa wa covid19.

Hivyo, Wizara imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa kuruhusu mechi kati ya timu ya Tanzania Prisons na Simba (Juni 28, 2020) kuchezwa na mashabiki baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kuthibitisha kwa maandishi kuwa watasimamia utaratibu wote wa Kanuni za Afya Michezoni kuzingatiwa wakati wa mchezo huo ikiwemo mashabiki kuingia wachache na kupangwa na kusimamiwa kukaa kwa kuachiana mita moja.

 

Pamoja na ahadi hiyo, iwapo kutakuwa na uvunjifu wowote wa taratibu uwanja huo utachukuliwa hatua kali zaidi ikiwemo kuzuiwa usitumike kabisa kwa michezo ya ligi kuu.

 

Aidha, Wizara inaendelea kuwakumbusha wadau wa michezo pamoja na mashabiki kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 unaoasababishwa na virusi vya Corona na kusisitiza kuwa hatua zitaendelea kuchukuliwa kwa viwanja vitakavyokiuka Mwongozo wa Afya michezoni.

Leave A Reply