Serikali yatahadharisha vyombo vya habari na matokeo batili ya uchaguzi mkuu

1.Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo),Assah Mwambene (kulia) akizungumza na wanahabari.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene (kulia) akizungumza na wanahabari.

2.Wanahabri wakifuatilia mkutano huo.

Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

3.Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

4.Mwambene (kulia) akitafakari kujibu maswali yaliyokuwa yameulizwa na wanahabari.Mwambene (kulia) akitafakari kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

IDARA ya Habari (Maelezo) imevitahadharisha vyombo vya habari nchini kuhusu kuchapisha au kurusha hewani matokeo ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaoendelea na kusema kuwa, kazi hiyo ni ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) pekee.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa idara hiyo, Assah Mwambene amesema kuwa hakuna taasisi nyingine yoyote yenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya uchaguzi na kufanya hivyo ni kuvunja sheria na kuongeza kuwa, vyombo vya habari vitakavyohusika kuchapisha matokeo yasiyotolewa na tume ya uchaguzi pia vitavunja sheria.

Amesema kuwa, vyombo vya habari vinaweza kuhatarisha amani iliyopo kwa kuweka taarifa zinazokinzana kuhusiana na matokeo hayo jambo linaloifanya idara yake iwakumbushe wanahabari kuhusu kutunza amani iliyopo bila kuchochea vurugu kwa kuzingatia matokeo yanayotolewa na tume pekee.

Mbali na hayo, Mwambene alisema amepata taarifa kuwa kuna chama kimoja kinataka kutangaza matokeo yake jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya tume ya uchaguzi.

(HABARI: Denis Mtima na Chande Abdallah / GPL)


Loading...

Toa comment