The House of Favourite Newspapers

Serikali Yatoa Siku 54 Magazeti Yote Tanzania Yasajiliwe Upya (Video)

0
Msemaji wa Serikali Dk Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza na wanahabari.
SERIKALI imetoa tamko rasmi likiyataka magazeti na majarida yote hapa nchini kusajiliwa upya kuanzia leo Alhamisi, Agosti 23 hadi hadi Oktoba  15, 2017 kwa mujibu wa sheria.
Msemaji wa Serikali  Dk Hassan Abbasi ameyaeleza hayo leo wakati akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Habari Maelezo, Posta jijini Dar es Salaam.
“Baada ya Oktoba 15, 2017 hakuna atakayeruhusiwa kuchapisha bila usajili”Amesema Dk Abbasi na kuongeza. Mfumo mpya wa utoaji wa leseni kwa machapisho yote umeanza rasmi leo ‘’
Amesema  taratibu zote za upatikanaji wa leseni zimewekwa katika tovuti   http://www.maelezo.go.tz
Mawasiliano kwa ajili ya ufafanuzi kuhusu utaratibu wa usajili ni 0622664606 na 0717312417 au kupitia [email protected]
TAARIFA YA SERIKALI KWA UMMA

VIDEO: Serikali Yaagiza Magazeti Yote Tanzania Kusajiliwa Upya Kabla ya Oktoba 15

Leave A Reply