The House of Favourite Newspapers
gunners X

Serikali Yatangaza Ajira 136 Mpya IAA, TAA, NECTA, TIE na NACTVET

0

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza jumla ya nafasi 136 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, kwa niaba ya taasisi mbalimbali za serikali. Fungua link kusoma zaidi hapa chini

Taasisi hizo ni pamoja na:

  • Institute of Accountancy Arusha (IAA)

  • Tanzania Airports Authority (TAA)

  • Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH)

  • National Examination Council of Tanzania (NECTA)

  • Tanzania Institute of Education (TIE)

  • Tanzania Library Services Board (TLSB)

  • National Council for Technical and Vocational Education and Training (NACTVET)

Kwa mujibu wa PSRS, wanahitajika wataalamu wenye uadilifu, uwezo wa kufanya kazi kwa matokeo na kujituma.

Nafasi nyingi: Wahadhiri Wasaidizi, ICT, Utawala na Dereva

Katika tangazo hilo, IAA ina nafasi nyingi zaidi, hasa kwa wahadhiri wasaidizi (Assistant Lecturers) katika fani mbalimbali kama:

  • Leadership & Governance

  • Tourism and Hospitality

  • Chinese Language

  • French Language

  • Records & Information Management

  • Programming na Cyber Security

  • Human Resource Management

  • Procurement & Logistics

  • Accounting & Finance

  • Insurance & Social Protection

  • Wildlife Management

Wengi wa waombaji wanatakiwa kuwa na:

  • Shahada ya kwanza yenye GPA kuanzia 3.5

  • Shahada ya Uzamili (Master) yenye GPA kuanzia 3.8

  • Kutoka taasisi zinazotambulika.

Aidha, zimetangazwa pia nafasi za:

  • Tutorial Assistants

  • Receptionists

  • Madereva (wenye leseni daraja C au E na uzoefu usiopungua mwaka mmoja)

TAA: Wataalamu wa Apron na Operesheni za Uwanja wa Ndege

Tanzania Airports Authority (TAA) inahitaji hasa:

  • Aircraft Marshallers (23)

Wataalamu hawa watakuwa na jukumu la kusimamia ndege zinapoingia na kutoka, usalama wa apron na uendeshaji wa vifaa.

Waombaji wanatakiwa kuwa na diploma katika fani zinazohusiana na utawala, rasilimali watu au biashara, na uelewa wa TEHAMA. Mafunzo maalum ya apron yatatolewa baada ya kuajiriwa.

COSTECH: Wataalamu wa ICT wanahitajika

COSTECH inatafuta:

  • ICT Officer – Systems Developer

  • ICT Officer – Network Administrator

  • Dereva

Wagombea wanapaswa kuwa na shahada katika TEHAMA, Uhandisi Kompyuta au Sayansi ya Kompyuta, pamoja na ujuzi wa mifumo na usimamizi wa mitandao.

NECTA: Maafisa Mitihani na Uchapaji

Kwa upande wa NECTA, nafasi zilizotangazwa ni pamoja na:

  • Printing Assistants

  • Examinations Officers kwa masomo kama:

    • Tourism & Hospitality

    • Music Performance

    • Fine Art

    • Performing Arts

Majukumu yao yanajumuisha usimamizi wa uandaaji, uchapaji, uchambuzi na usahihishaji wa mitihani ya kitaifa.

Tarehe ya mwisho ya maombi

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kabla ya 11 Januari, 2026.

THE BEAST: NGOME ya JESHI INAYOTEMBEA – NI GARI la RAIS wa MAREKANI…📍 USA

Leave A Reply