Serikali Yatoa Kanuni 8 za Kujikinga na #COVID19

 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kusimamia na kusisitiza utekelezaji wa tahadhari ya magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na ya kuambukiza yakiwemo ya milipuko ikiwemo tishio la ugonjwa wa COVID-19 linaloikabili dunia kwa ujumla.

 

 

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imetaja mambo nane ya kuzingatia kujikinga na magonjwa hayo;

a) Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi tiririka na sabuni,

b) Kutumia vipukusi (sanitizer) mara kwa mara ikiwemo pale ambapo hakuna maji safi tiririka na sabuni,

c) Kufanya mazoezi mara kwa mara,

d) Kuwalinda wale wote walio katika hatari kama wazee, watu wanene, na wenye magonjwa ya muda mrefu,

e) Kupata lishe bora ikiwemo matunda na mbogamboga,

f) Matumizi ya tiba asili zilizosajiliwa na baraza la tiba asili na kama inavyoelimishwa na wataalamu husika,

g) Kuvaa barakoa pale shughuli zako za siku hiyo zinapokuwa zinakupelekea kupata au kutoa huduma kwa mwingine aliyeko umbali wa chini ya mita moja ili kupunguza hali hatarishi ya kupeleka mate toka
kwa mmoja kwenda kwa mwingine. Inashauriwa kuvaa barakoa uliyotengeneza mwenyewe,

h) Kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya mara uonapo dalili za maradhi ili watoa huduma wapate nafasi nzuri zaidi ya kutibu.

 

 

Aidha, wizara imewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kupima afya yake mara kwa mara ili kutambua hali zao za kiafya na endapo watatambuliwa kuwa na ugonjwa au vihatarishi vya magonjwa mbalimbali yakiwemo yasiyoambukiza basi watashauriwa kuwajibika kutumia huduma za afya au vinginevyo ili kufanya miili yao uwe imara zaidi.

Toa comment