Serikali Yatoa tamko kuhusiana na tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Marburg

Serikali kupitia Wizara ya Afya inayoongozwa na Waziri Jenista Mhagama, imetoa tamko rasmi kuhusiana na tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera.
Kupitia taarifa yake, Wizara ya Afya imesema kuwa imechukua hatua za haraka ikiwemo uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Wizara pia imewahakikishia wananchi kuwa mifumo ya ufuatiliaji imeimarishwa na ufuatiliaji wa hali unaendelea kwa ukaribu.