The House of Favourite Newspapers

Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu huduma za ziada za kielektroniki.

0

mawasilianoKutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Mawasiliano, Samson Mwela, Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prisca Ulomi na mkuu wa kitengo cha sheria katika wizara hiyo, Veronica Sudayi.

2.Viongozi hao wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).Viongozi hao wakiwa makini kusikiliza na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

3.Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Sayansi Teknolojia na Mawasiliano Tanzania, leo Ijumaa imetoa taarifa juu ya kanununi mpya za huduma za ziada za mwaka 2015 za sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ya mwaka 2010.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, msemaji wa wizara hiyo, Prisca Ulomi, amesema kuwa hududuma za ziada ni zile huduma za mawasiliano za kielektroniki zinazotolewa kupitia mitandao zaidi ya huduma za msingi za mawasiliano ya kawaida.

Mlomi amefafanua kuwa, Serikali kupitia wizara yake hiyo, ilitunga kanuni za huduma za ziada za mwaka 2015 (Value Added Services-‘VAS’ Regulation) na kuzitangaza kwenye gazeti la serikali la Agosti 7, mwaka huu na kupewa GN. Namba 320 huku sheria hizo zikiwa ni za mawasiliano ya kielektroniki na posta ya mwaka 2010 iliyotungwa na kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema, katika huduma hizo mtumiaji anaweza kujiunga na kujiondoa kupata huduma hizo za ziada kwa kutumia kanuni na sheria, endapo mtoa huduma hatozingatia taratibu zilizowekwa, anawajibu wa kupata adhabu kwa kukiuka matakwa ya kanuni hizo.

Amefafanua kuwa, kwa kupitia kanuni hizo za VAS, zinamtaka mtoa huduma za ziada kutoa taarifa kamili na sahihi kuhusu huduma za ziada kwa lugha rahisi na ya uwazi ambapo ataweza kutoa masharti na vigezo vya huduma zake ikiwemo gharama kwa njia ya kielektroniki na kudurufu (printed and electronic formats).

Amefafanua kuwa, mtoa huduma endapo ataamua kubadilisha huduma yake ya kielektroniki, mtumiaji atatakiwa apatiwe taarifa kamili kuhusu masharti ya uhamaji, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika utoaji  wa huduma hizo na gharama endapo zitajitokeza.

Aidha kwa upande mwingine, kanuni hizo zinamtaka mtoa huduma kuweka mfumo wa kuwezesha huduma za ziada kwa mtumiaji kujiunga au kujiondoa ambao ni rahisi na wa uwazi kwa kutumia teknolojia inayofaa ikiwemo ujumbe mfupi wa maneno (SMS), huduma ya sauti au namba maalum.

Mlomi ametoa rai kwa watoa huduma za ziada kuendelea kuzingatia kanuni na sheria katika kuwapatia wateja wao huduma zenye ubora na viwango vinavyotakiwa na watumiaji ili kuhakikisha wanapatiwa huduma stahiki na waliyoomba huku akitaja kuwa kanuni hizo mpya zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambayo ni www.mst.go.tz

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply