The House of Favourite Newspapers

SERIKALI YAZUA BALAA DAWA ZA NGUVU ZA KIUME!

Afisa uhusiano wa TFDA Gaudensia Simwanza .

SIKU chache baada ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kusa­jili na kuthibitisha dawa tano za asili ikiwemo Ujana inayotibu nguvu za kiume, imebainika kuwa suala hilo limezua balaa la aina yake mitaani kwa wanandoa kuvutana kwa ajili ya kuzi­saka dawa hizo huku pia baadhi ya watu waliokuwa wakiuza dawa za tatizo hilo wakilalamikia kukimbiwa na wateja.

UCHUNGUZI WA UWAZI

Uwazi liliingia mtaani kufanya uchunguzi wa mapokeo ya watu wa kada mbalimbali ambao walitoa maoni yao kuhusu ‘neema’ ya ujio wa dawa hiyo katika jamii na kubaini jinsi ilivyozua balaa katika familia mbalimbali.

 

Katika maeneo ambayo Uwazi lilifika jijini Dar, ilibainika kwamba, wanandoa wengi wapo kwenye mshikemshike nguo kuchanika wakivutana katika kutafuta suluhu ya tiba kwani tatizo hilo limekuwa likiwatesa kwa muda mrefu.

“Mimi nilioana na mke wangu miaka kumi iliyopita, lakini kimsingi sikuwahi kuifurahia ndoa yangu. Tumevutana sana na mke wangu. Kuna wakati ilifikia mahali hadi akaamua kuondoka nyumbani. Baa­daye tulifanya mazungumzo na wazazi, akarudi.

“Tumeendelea kuishi hivyo na mimi nikawa ninajaribu kutumia dawa mbalim­bali za asili bila mafanikio. “Utaambiwa mara sijui kuna dawa hii, mara utaambiwa kuna dawa ile, lakini zote hazikunipa matokeo mazuri,” alisema mkazi mmoja wa Bunguruni jijini Dar huku akiomba hifadhi ya jina.

 

BAADA YA SERIKALI KUTHIBITISHA

Mkazi huyo wa Buguruni alizidi kueleza kuwa, mara baada ya serikali kutangaza kuzisajili na kuzithibitisha dawa hizo tano za asili, mkewe amechachamaa upya na kumtaka ahakikishe anazitafuta na kuzipata ili angalau naye afurahie tendo la ndoa.

“Yaani huwezi kuamini, badala ya kuwa furaha, imekuwa tena ugomvi. Nimemwambia ninajaribu kufuatilia kwa makini ili ninunue maana kimsingi serikali yenyewe imetan­gaza tu kuzisajili, lakini haikusema zinapatikana wapi.

“Sasa wakati mimi niki­wa ninatafuta suluhu, yeye (mkewe) anaona kama vile labda silitilii maanani. Sasa ukirudi tu nyumbani kabla hamjaongea lolote ishu kwanza ni hizo dawa,” alisema mwa­nanchi huyo.

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile.

 

TATIZO NI KUBWA

Mbali na mkazi huyo wa Buguruni, Uwazi lilibaini kwamba, wanandoa wengi wame­kuwa kwenye taharuki ya aina yake baada ya serikali kuzisajili dawa hizo za asili kwani wapo kwenye msuguano mkubwa kwa wanaume kuahidi kuzisaka, lakini wanawake hawawaelewi.

“Unajua kabla ya kutangazwa kwa dawa hizi, kama unavyojua jambo lenyewe hili ni la siri, wengi walikuwa wakijitibia kwa dawa za kienyeji, lakini bahati mbaya sana wengi walikuwa wakikosa tiba sahihi. Baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari, wa­nawake wamewachachamalia waume zao bila kujua wapi zinapatikana,” alisema Abdu Machao wa Sinza jijini Dar.

WANANDOA, WACHUMBA WAACHANA

Uchunguzi huo uliendelea ku­baini kwamba, katika miaka ya hivi karibuni, tatizo la nguvu za kiume limekuwa kubwa na kusababisha wachumba wen­gi kuachana wakiwa katika hatua za awali, sambamba na wandoa.

Akida Nduli, mkazi wa Mbagala jijini Dar, akizungum­za na Uwazi, alisema kuwa, kwa miaka ya hivi karibuni, tatizo hilo limekuwa kubwa ki­asi cha kumtisha kwa sababu hadi sasa, ameshashuhudia ndoa nyingi zikivunjika, achilia mbali wale wanaoachana wakiwa wachumba kutokana na tatizo hilo la nguvu za kiume.

“Kwa kweli tatizo ni kubwa mno, nime­shuhudia ndoa nyingi sana zikivunjika. Kwa upande wa wachumba ndiyo usiseme. Wao wanaachana tu maana wengi wao wanaona hakuna sababu ya kuendelea na uhusiano wakati wameshaona tatizo mapema,” al­isema Nduli.

NABII APIGILIA MSUMARI

Nabii wa Kanisa la Jerusalem lililopo Kitunda jijini Dar, James Nyakia, akizungumza na Uwazi kuhusu ukubwa wa tatizo la nguvu za kiume, alisema kuwa, katika shughuli zake za kinabii, amekuwa akikutana na kesi nyingi za wanandoa zinazotokana na tatizo la nguvu za kiume.

“Kwa kweli ni tatizo. Miongoni mwa saba­bu kubwa zinazosababisha watu waingie kwenye migogoro ya ndoa ni suala la nguvu za kiume. Kesi nyingi zinazokuja ni huenda mwanamke amesaliti ndoa kwa sababu ya tatizo hilo au mwanamke anamkimbia mumewe kwa sababu hiyo au ugomvi wa mara kwa mara kwa mwanamke kutofura­hia tendo,” alisema nabii huyo.

Aidha, nabii huyo alisema kuwa, ana imani na dawa hizo zilizotangazwa na serikali kwamba huenda zikasaidia kuleta ufumbuzi wa tatizo hilo, lakini pia akawa­taka wanaume kuzingatia vyakula vya kula kwani tatizo hili linachangiwa pia na ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi pamoja na sukari.

“Dawa zimeshathibitishwa na serikali zinaweza kusaidia ni wao tu sasa kuamua kusuka au kunyoa kwa maana ya kuzitafuta au kuendelea kuteseka. Lakini ni vyema wakapunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta na pia wakajenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuifanya miili yao iwe na nguvu ya kutosha,” alisema Nabii Nyakia.Supu ya pweza

WAUZA SUPU YA PWEZA WANENA

Uwazi lilizungumza na wauzaji mbalimbali ,Wauza supu ya pweza wengi waliozungumza na Uwazi walisema kuwa, wao wamekuwa wakiuza bidhaa hiyo wakiamini ni kama kiburudisho, lakini wame¬jikuta wengi wakisambaziana habari kuwa inasaidia nguvu za kiume hivyo kitendo cha serikali kutangaza dawa hizo tano za asili, kimewafanya wateja waliokuwa wananunua kwa ajili ya kuongeza nguvu waache kununua.

“Wengi sasa hivi wanatafuta hizo dawa za serikali. Kidogo idadi kwetu imepungua,” alisema muu¬zaji wa supu ya Pweza anaye¬fanya shughuli zake Mwenge jijini Dar.

Vumbi la kongo

VUMBI LA KONGO

Kwa upande wao wauzaji wa Vumbi la Kongo, walisema kuwa, nao wameathirika na kauli ya serikali kuzithibitisha dawa tano za asili ikiwemo Ujana kwani wa¬likuwa wakifanya sana biashara kabla.

TUMEFIKAJE HAPA?
Machi 13, mwaka huu, Msajili wa Baraza la Tiba za Asili na Mbadala, Dk Ruth Suza, katika mkutano na waandishi wa habari, alitan¬gaza kuzithibitisha dawa tano za asili ikiwemo hiyo ya Ujana inayotibu nguvu za kiume.

Mbali na Ujana, dawa nyingine alizozitaja ni IH Moon, Coloidal Silver, Sudhi na Vatari zinazotibu magonjwa mbalimbali.

Pia Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza alizitaja dawa nyingine mbili za aina ya Sildenafil na Tadalafil zinazotoka nje ya nchi kwa ajili ya kusaidia tatizo hilo la nguvu za kiume.

Awali, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile (pichani uk. 3) katika mkutano huo, alimuagiza katibu mkuu wa wizara yake, Dk Mpoki Ulisubisya kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya utafiti wa afya ya uzazi kwa wanaume ili kubaini sababu na pia kujua ongezeko la upungufu wa nguvu za kiume ni kubwa kwa kiasi gani nchini.

Waziri huyo alitoa agizo kwa waganga wote wa tiba asili na tiba mbadala kuacha mara moja kutoa matangazo yao mbalimbali kupitia vyombo vya habari na mabango ya barabarani kuhusu tiba ya ugonjwa huo.

Comments are closed.