The House of Favourite Newspapers

Mke wa Dkt. Slaa Atajwa Kesi ya Lulu Kifo cha Kanumba

0
Elizabeth Michael ‘Lulu’

KESI inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayedaiwa kumuua muigizaji mwenzake, Steven Kanumba, bila kukusudia, iliendelea leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kuahirishwa baada ya shahidi upande wa utetezi kutofika mahakamani.

Akiwasilisha maombi, wakili anayeongoza upande wa utetezi, Peter Kibatala, aliiomba, mahakama kupokea ushahidi wa maandishi kwa madai kuwa shahidi yupo nje ya nchi. Kibatala amesema mashahidi huyo anayemtetea Lulu, Josephine Mshumbusi ambaye ni mke wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Slaa yuko nchini Canada.

Baada ya maelezo hayo ya Kibatala, kulitokea mvutano mkali mahakamani hapo kati ya upande wa Jamhuri na upande wa utetezi ambapo Jamhuri ilikataa kupokelewa ushahidi huo kwa madai kuwa mahakama haiwezi kupokea ushahidi wa maandishi wakati aliyeuandika hayupo.

Aidha Wakili wa Serikali, Faraja George, alimtaka Kibatala asijivishe kofia mbili (wakili na shahidi wa Lulu) kwa kutaka kusoma ushahidi huo mahakamani.

Jaji Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo alikataa kupokea ushahidi huo na kuwataka upande wa utetezi kumleta askari polisi Sajent Nyangea kusoma maelezo ya Mshumbusi huku jaji huyo akiiahirisha kesi hadi Oktoba 25 mwaka huu.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

VIDEO: LULU KORTINI LEO

Leave A Reply