The House of Favourite Newspapers

SHAHIDI AKWAMISHA KESI YA TIDO KISUSTU

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam itaendelea kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, Juni 8, mwaka huu.

 

Wakili wa Takukuru, Leonard Swai, leo mei 18, 2018 amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka leo, lakini shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi alikuwa na udhuru.

 

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Juni 8,2018 ambapo mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi.

 

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi ambao ni Afisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

 

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya mamilioni ya shilingi. Tido anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 akiwa UAE, aliisababishia TBC hasara ya Sh887,122,219.19. Tido anatetewa na Wakili Ramadhani Maleta na yupo nje kwa dhamana.

Comments are closed.