The House of Favourite Newspapers

Shambulio la Kigaidi la 9/11, Miaka 16 Baadaye Bado Osama Hatasahaulika

0

Osama bin Laden enzi za uhai wake.

Osama.

Taswira ya maghorofa ya World Trade Centre baada ya kushambuliwa.

Hali ilivyokuwa Septemba 11, 2001.

Asubuhi ya Jumanne, Septemba 11, 2001, dunia ilisimama kufuatia mashambulizi ya kutisha yaliyolenga kwenye majengo marefu zaidi duniani kwa wakati huo ya kituo cha biashara, World Trade Centre (WTC) jijini New York, Marekani na kusababisha vifo vya takribani watu 2,997 huku wengine zaidi ya 6,000 wakijeruhiwa, sambamba na hasara kubwa ya mabilioni ya fedha.

‘Mastermind’ wa tukio hilo ambalo halitasahaulika, alikuwa ni Osama bin Laden, kiongozi wa Kundi la Kigaidi la Al Qaeda na wakati Marekani ikiadhimisha miaka 16 leo tangu kutokea kwa tukio hilo, simulizi ya Osama bado ipo midomoni mwa wengi, kutokana na madhara aliyoyasababisha kwa Wamarekani.

Leo maelfu ya Wamarekani, wanajumuika kwenye ukumbi wa makumbusho ya shambulio, National Memorial Museum jijini New York kwa ajili ya kutoa heshima na kuwakumbuka wahanga wa tukio hilo lililoacha maumivu makubwa kwa Wamarekani na dunia nzima kwa jumla.

 

Leave A Reply