The House of Favourite Newspapers

Shambulio la Sinagogi Jerusalem: Saba Wauawa katika Shambulio la Risasi

0
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametembelea eneo la shambulio.

Watu saba wamepigwa risasi na kufa katika sinagogi lililopo mashariki mwa mji wa Jerusalem, ikiwa ni idadi kubwa ya watu waliouliwa katika shambulizi la aina hii kwa miaka ya hivi karibuni.Takriban watu watatu zaidi wamejeruhiwa.

Tukio hilo limetokea katikaeneo la mji wa Jerusalemu linalofahamika kama Neve Yaakov majira ya saa mbili na robo kwa saa za eneo.

Polisi imemuelezea mshambuliaji kama “gaidi” na kuongeza kuwa ameuawa.

Vyombo vya habari vimemtambua mshambuliaji kama mwanaume Mpalestina kutoka Jerusalem Mashariki.

Polisi wa Israel wamesema Jumamosi kwamba wamewakamata watu 42 kuhusiana na ufyatuaji wa risasi.

Akisungumza katika eneo la shambulizi, kamanda wa polisi wa Israeli Kobi Shabtai aliita “moja ya mashambulio mabaya zaidi ambayo tumekabiliana nayo katika miaka ya hivi karibuni “.

Waumini wa Israeli walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya maombi katika mwanzo wa sabato ya Wayahudi katika sinagogi katika makazi ya Wayahudi na walikuwa wanaondoka wakati mtu mwenye silaha alipoanza kuwafyatulia risasi. Police inasema kuwa baadaye maafisa walimpiga risasi ya kichwani akafa.

Leave A Reply