Shambulio laua watatu kliniki ya wazazi Colorado, Marekani

marekani (1)Majeruhi wakiokolewa.marekani (2)Jeshi la Polisi la Colorado likitoa msaada kwa waathirika wa shambulio hilo.marekani (4)Mtuhumiwa, Robert Lewis Dear (miaka 59) baada ya kujisalimisha.
marekani (3)..hali ilivyokuwa.
marekani (5)…uokoaji.marekani (6)Mama huyu akisaidiwa kutolewa eneo la tukio.marekani (7)Magari ya polisi wakiwa kwenye doria kumsaka mtuhumiwa wa shambulio hilo.marekani (8)Ofisa wa Polisi, Garrett Swasey (miaka 44) aliyefariki kwenye shambulio hilo.
Shambulizi marekani (1)Mmoja wa waathirika wa shambulio hilo akihojiwa na vyombo vya habari.
Shambulizi marekani (2) Polisi wakiwa kwenye doria.Shambulizi marekani (3)Polisi wakiwa kwenye doria.Shambulizi marekani (4)

Colorado, Marekani

WATU watatu akiwemo askari polisi mmoja wamefariki kwenye tukio la kushambuliwa kwa kumiminiwa risasi kwenye kituo kimoja cha kliniki ya wazazi kilichopo Mji wa Colorado, Magharibi mwa nchi ya Marekani usiku wa kuamkia leo.

Katika shambulio hilo watu wengine tisa wameripotiwa kujeruhiwa, japo hakuna majeruhi walio katika hali mbaya.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi wa mjini Colorado walianza kumsaka mtuhumiwa aliyetambuliwa kwa jina la Robert Lewis Dear (miaka 59) ambaye saa tano baadaye, yeye mwenyewe alijisalimisha kwenye jeshi hilo wakamtia nguvuni.

Ofisa wa Polisi aliyefariki ametambuliwa kwa jina la Garrett Swasey (miaka 44) ana mke na watoto wawili.

Meya wa Mji wa Colorado, John Suthers amesema kuwa, inawezekana shambulio hilo lilipangwa siku chache kabla, na kwamba liliwalenga hasa wakina mama na watoto amabao huwa wanakwenda kwenye kituo hicho cha kliniki kupata matibabu na huduma zingine za kiafya.

Loading...

Toa comment